Habari

Watanzania naomba mniombee – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa anaomba siku zote Watanzania wamuombee ili ashinde vita ya uchumi.

Rais Magufuli ameyazungumza hayo Manyara wakati akizungumza na wakazi wa Simanjiro ambapo amesema kuwa Tanzania haikuumbwa kwaajili ya mafisadi.

“Ndio maana naomba siku zote ndugu zangu Watanzania naomba mniombee naomba tusimame pamoja ili tusimame pamoja tukashinde vita hii kwa maslahi ya Watanzania hasa Watanzania masikini. Leo nimekuja hapa ninajua nimekuja kufungua barabara nitaifungua lakini ngoja tuzungumzie suala la Tanzanite kwanza,” amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania haikuumbwa kwaajili wa mafisadi, Tanzania imeumbwa kwaajili ya wanyonge.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents