Burudani

Watanzania wamejawa na ujuaji na chuki- Baraka da Prince

Msanii wa muziki bongo, Baraka da prince ametamba na “acha niende”, huku akisema amewataja watanzania kuwa kama wajuaji na wenye chuki.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Baraka amefunguka kwa kuandika, “Tangu ninazaliwa sijapata kuona nchi yenye wajuaji wengi kama #TANZANIA..tangu nazaliwa sijawahi kupata kuona nchi yenye binadamu wenye chuki baada kuona mtu kafanikiwa kama #TANZANIA siku hizi mashabiki wamekuwa walimu wa mashahiri na wamekuwa wajuaji kuliko hata sisi tunaoimba mziki.”

Hatua hiyo ya kuandika hayo, imetokana na baadhi ya mashabiki kukosoa kazi mpya ya msanii Darassa CMG, iitwayo ‘Hasara roho’ iliyotoka hivi karibuni kuwa sio nzuri kama ilivyo kwa kazi ya “muziki”.

Baraka pia amezikosoa page zinazojiita page za udaku zilizopo kwenye mitando hasa Instagram kwa kukosoa kazi za wasanii na kutaka kurudisha mafanikia ya watu nyuma.

“Ujue mziki sio kitu ki rahisi kama watu wengi humu ndani mnavyodhania na sio lazima kila kitu kiwe sawa au mapokezi kufanana na kilichopita nyuma…Hakuna kitu kinaboa Duniani kama mtu unapoteza muda wako na nguvu nyingi kuwekeza katika kazi yako au kupigania mafanikio yako,alafu kinakuja kijimtu sijui hata kimetoka wapi kinaanza kuponda kile kitu ulichopoteza muda na nguvu nyingi na pesa pia Nyie watu wajuaji mnaboa kinoma…Tungeni zenu Nzuri na video zenu Nzuri tuzione,Hao Hao kesho ndio utawasikia wakiimba kama wimbo wa taifa”alimaliza kwa kuandika hivyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents