Michezo

Watanzania watatu wapata shavu CAF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF} limewateua watanzania watatu kuwa maofisa waandamizi katika kusimamia mchezo wa Kundi A hapo kesho utakaowakutanisha Ghana na Gabon kwenye uwanja wa Port Gentil kwenye michuano ya Afcon U-17


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF}

Watanzania hao ni Mwesigwa Joas Selestine, ambaye atakuwa Kamishna wa mchezo huo, Frank John Komba kupewa nafasi ya mwamuzi msaidizi pamoja na Dk. Paul Gaspel Marealle kushika kitengo cha kitaalamu cha uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia dawa za kusisimua misuli.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania {TFF} imewapongeza viongozi hao waliochaguliwa na CAF huku wakiwatakia kila la kheri katika kutimiza majukumu waliyopangiwa kesho na baadaye hasa ikizingatiwa kuwa fainali zijazo za vijana kama hizi, zitafanyika Tanzania mwaka 2019.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents