Watatu Polisi kwa wizi wa gari kanisani

Wakazi watatu wa jijini wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuiba gari lililokuwa limeegeshwa nje ya kanisa la Mt. Joseph na muumini Gregory Viscent (34), aliyekuwa amekwenda kusali.

Wakazi watatu wa jijini wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuiba gari lililokuwa limeegeshwa nje ya kanisa la Mt. Joseph na muumini Gregory Viscent (34), aliyekuwa amekwenda kusali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kanda Maalum Dar es Salaam, Faustine Shilogile amesema kuwa tukio hilo limetokea jana saa 7 mchana, juzi, mtaa wa Sokoine kwenye viwanja vya kanisa la Mt. Joseph.

Amesema muumini huyo akiwa na gari lake namba T 170 AGP aina ya Toyota Cresta aliegesha gari nje ya kanisa hilo na kuingia kusali na alipotoka alikuta gari hilo halipo.

Amesema polisi baada ya kupata taarifa walifanya upelelezi na kulinasa gari hilo likiwa nyumbani kwa Omary Mbembeni (50), mkazi wa Tabata Kimanga jana saa 4 usiku.

Amesema pia jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa Mohamed Juma (42) na Samora Dismas (23), kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Shilogile ameongeza kuwa, gari hilo lilikutwa likiwa bado halijabadilishwa namba na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents