Michezo

Watatu wala shavu la Basketball

Wachezaji watatu wa mpira wa vikapu, Aliphaes Kisusi, Sunday Edward na Evance David wanatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda Marekani kushiriki mashindano yalioandaliwa na kampuni ya coca cola chini ya chapa yao Sprite, nchini humo.

Vijana hao watatu kutoka Tanzania wataungana na wenzao kutoka nchi nyingine za Afrika ambapo wataunda timu ambayo itacheza dhidi ya timu za Marekani.

Wachezaji hao watatu walipatikana katika kliniki maalumu iliyoendeshwa na mchezaji wa zamani wa ligi kuu ya kikapu Marekani (NBA) Steve Smith aliyewahi kuchezea Atlanta Hawks na Miami Heat pamoja na mkufunzi w kimataifa wa NBA Martin Coonlon.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi bendera kwa wachezaji hao, Mwenye kiti wa baraza la michezo la Taifa(BMT), Idd Kipingu aliwataka wachezaji hao kufanya vizuri katika kliniki hiyo ili kuitangaza nchi zaidi kimataifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents