Habari

Watatu washikiliwa kwa tuhuma za kuchoma ofisi za CHADEMA, Arusha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watumishi watatu wa CHADEMA kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kuchoma moto ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini, zilizoteketea Agosti 14, 2020, na kusababisha uharibifu wa mali wa thamani ya zaidi ya Milioni 5 baada ya tathmini kufanyika.

Image

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Septemba 3, 2020, na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Salum Hamduni, ambapo amesema kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea, uchunguzi wa kina ulifanyika kuwabaini na kuwakamata watu wote waliohusika katika tukio hilo ambapo Agosti 19 alikamatwa mlinzi wa Ofisi hiyo aitwaye Deogratius Malya.

Mbali na huyo Jeshi hilo pia limemkamata Leonard Cathbert Ntukula, ambaye ni Dereva wa CHADEMA na Mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam, pamoja na Prosper Masatu Makonya, ambaye ni Afisa mhamasishaji wa CHADEMA Makao Makuu na Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam, ambao wote hao walikamatwa kati ya Agosti 28 na 29 mwaka huu.

Aidha Kamanda Hamduni ameongeza kuwa, baada ya kukamilisha upelelezi, jalada la kesi hiyo limepelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kulisoma na kulitolea maamuzi ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuandaa hati ya mashtaka, na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents