Aisee DSTV!

Wateja wa DStv waendelea kupeta na promosheni ya Tia kitu, pata vituz

Dar es Salaam April 4, 2019. Kwa mara nyingine tena kampuni inayoongoza kwa huduma bora za vinga’muzi nchini, DStv imetangaza washindi wengine 15 wa droo ya 6 ya Promosheni yao mahsusi inayoendelea nchi nzima maarufu kama “ Tia Kitu pata vituz”.


Akizungumza na waandishi wakati wa kuwatangaza washindi wa droo ya wiki ya sita katika makao makuu ya ofisi za MultiChoice Tanzania zilizopo Kinondoni Dra es Salaam, Meneja Rasilimali watu wa kampuni hiyo bi. Tike Mwakitwange alieleza kuwa Promosheni
hiyo ni ya wazi kwa wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla havijakatika.“Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na fursa ya kujishindia kifurushi kile kile alicholipia kwa
muda wa miezi miwili”, alisema Tike.


Mpaka sasa wameshapatikana jumla ya washindi 90 kupitia promosheni ya Tia Kitu , pata vituz kutoka maeneo tofauti tofauti kote nchini ikiwamo Shinyanga, Mtwara, Kagera, Mbeya , Arusha na hapa Dar es Salaam. Hii ni wazi kuwa huduma zinazotolewa na DStv ni bora na zisizo na kifani, alieleza Tike. Aidha amesema kuwa washindi hao 15 wamejinyakulia malipo ya miezi miwili ya vifurushi
vile vile walivyolipia ili kuendelea kufaidika na burudani kadha wa kadha kupitia king’amuzi chao pendwa cha DStv.
Naye bi. Witness Stanslaus moja kati ya washindi wa droo ya wiki ya sita kutokea jijini Dar es Salaam amewapongeza na kuwashukuru DStv kwa kuendelea kuwajali wateja wake,
“Sikutegemea kuibuka na ushindi huu, kwa kweli nimefurahi sana na Zaidi ninafurahishwa na jitihada za DStv katika kutujali wateja wake na kuhakikisha inatupatia huduma bora Zaidi siku hadi siku”, alisema Witness.
Pia amewapa ujasiri wateja wengine wa DStv kulipa kwa wakati ili kujipatia fursa hiyo ya
kuingia kwenye droo hiyo ya kushinda miezi miwili bila malipo kwa wiki zilizosalia.
 1.Photos: Meneja Rasilimali watu wa MultiChoice Tanzania bi. Tike Mwakitwange (Kulia)
Akichezesha droo ya wiki ya sita ya Promosheni ya Tia Kitu pata vituz, Kulia ni Benson Urio
wa kitengo cha Teknohama. Promosheni hiyo ni ya muda wa wiki 8 ambapo jumla ya
washindi 120 watapatikana.
2.Photos: Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Jehud Ngolo (kushoto)
akizungumza kwa umakini na Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya wakatiwa droo ya wiki ya sita ya promosheni ya Tia kitu, pata vituzi. Promosheni hiyo ni kwa wateja
wanaolipia kwa wakati kabla vifurushi vyao havijakatika hivyo kupata fursa ya kushinda
kifurushi cha miezi miwili. Promosheni hiyo ni ya muda wa wiki 8 ambapo jumla ya washindi
120 watapatikana.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW