Wateja wa NMB sasa kuweka fedha kupitia M-Pesa

Benki ya NMB leo imeweka historia kwa kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha wateja wake nchini kuweza kuweka amana zao kupitia mawakala zaidi ya 40,000 wa M-Pesa Nchi nzima. Pia wateja wa NMB wataweza kutuma fedha kutoka NMB kwenda MPESA. NMB na Vodacom zimezindua huduma hiyo rasmi leo hii kwenye makao makuu ya NMB.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakitia sahihi katika mkataba kam ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB na Vodacom wakishuhudia.

Sasa mtu yeyote au wateja wa NMB hawatahitaji kwenda ndani ya benki ili kuweka fedha kwenye akaunti kwani sasa wataweza kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB bila kwenda tawini. Pia sasa wateja zaidi ya 800,000 wa NMB mobile wataweza kutuma fedha kwenda MPESA.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw.Mark Wiessing, alisema “Ni huduma ya aina yake ambayo itawezesha mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki kufanyika kwa urahisi na haraka, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini”.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakibadilishana mkataba kama ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB wakishuhudia.

Akizungumza kwa niaba ya Vodacom, Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt, amesema, “Hii ni hatua nyingine ambayo tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma ya M-Pesa kwa kushirikiana na benki ya NMB ambapo kwa kufanya hivyo itaruhusu wateja wa NMB kuweza kuweka amana zao kwenye akaunti zao kwa urahisi zaidi. Wakati huo huo, tunawaleta wateja wa benki ya NMB karibu na akaunti za benki zao kwa kuwezesha pesa kutoka benki kwenda M-Pesa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents