Habari

Watendaji wa Mahakama ya Tanzania watakiwa kuimarisha utendaji kazi

By  | 

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi awataka watendaji wa Mahakama ya Tanzania kuimarisha utendaji kazi na kusimamia mashauri yote kusikilizwa kwa wakati.


Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi

Pro.Palamagamba ameyasema hayo baada ya kufanya ziara katika ofisi za Mahakama ya Tanzania na kusema kuwa serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania.

“Tutambue kuwa zama zimebadilika tuimarishe utendaji wetu wa kazi, ili tuendane na ajenda ya serikali yetu ya awamu ya tano na dhamira ya Rais wetu kutokomeza vitendo vya rushwa na ufisadi kwa Watumishi na wananchi wote, kuimarisha uadilifu na uwajibikaji,” alisema Prof. Kabudi.

“Mahakama ina nafasi kubwa kuhakikisha ina imarisha inasimamia ipasavyo Watumishi wake ili waendane na malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kutokomeza rushwa na kuimarisha uadilifu na ufanisi katika kazi.”

Na Emmy Mwaipopo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments