Habari

Picha: Watetezi wa haki za binadamu nchini Kenya wakamatwa nje ya ubalozi wa Uganda

Watetezi wa haki za binadamu wanne wa Kenya wamekamatwa nje ya ubalozi wa Uganda jijini Nairobi asubuhi muda mfupi kabla ya kuwasilisha taarifa yao kwa vyombo vya habari kuhusiana na ukatili wa polisi dhidi ya upinzani nchini Uganda.

Wanaharakati hao ambao kwa sasa wanashikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa na polisi ni pamoja na Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika, Hussein Khalid pamoja na mwandishi wa habari Yassah Musa.

Image caption: Mtetezi wa haki za binadamu na Mkurugenzi wa Haki Afrika -Hussein Khalid akiwa amelala chini mbele ya polisi.




Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents