Soka saa 24!

Wateule wa Tanzania Music Awards watajwa!

Wateule wa Tanzania Music Awards 2011 watajwa

Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imetangaza wateule watakaowania tuzo za muziki za Kilimanjaro huku wasanii 20% na Linah wakiongoza baada ya kupendekezwa katika vipengele vitano.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Meneje wa bia ya Kilimanjaro ambao ndio waratibu wa tuzo hizo, George Kavishe alisema wateule hao waliteuliwa kwenye academy iliyofanyikwa wiki iliyopita.

Menejawa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, Angelo Luhala mratibu wa tuzo za kilimanjaro toka basata na mkaguzi wa tuzo toka INNOVEX
Menejawa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, Angelo Luhala mratibu wa tuzo za kilimanjaro toka basata na mkaguzi wa tuzo toka INNOVEX

Msanii 20% ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake za Tamaa mbaya na Ya nini Malumbano ameteuliwa kwenye tuzo ya Msanii bora wa kiume pamoja na Ali Kiba, Barnaba, Diamond, AY na Belle 9.

Aidha msanii huyo pia ameteuliwa kwenye tuzo ya Mwimbaji bora wa kiume pamoja na barnaba, Ali Kiba, Banana Zorro, Belle 9 na Diamond. 20% ambaye anatamba pia na filamu yake ya Furaha iko wapi, ameteuliwa tena kuwania tuzo ya Wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo wake wa  Ya nini malumbano na Tamaa mbaya.

Wengine wanaowania tuzo hiyo  na nyimbo zao zinazoshindanishwa zikiwa kwenye mabano ni Gelly wa Rymes Feat. AT, Ray C (Mama Ntilie), Sam wa Ukweli (Sina raha), Chege, Temba Feat Wahu (Mkono Mmoja) na Tip Top Connection (Bado tunapanda).

20% pia ameteuliwa kuwania tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo ambapo anawania pamoja na Barnaba, Lady Jaydee, Mrisho Mpoti na Mzee Yusuph. Tuzo nyingine anayowania ni ya wimbo wa Afro Pop kupitia nyimbo zek za Ya nini Malumbano na Tamaa mbaya. Wengine ni Gelly wa Rymes feat AT, Ray C (Mama Ntilie), Bon Junior (Oyoyo), na Diamond (Mbagala).

Kwa upande wa Linah ambaye ni zao la THT ameteuliwa kuwania tuzo ya Msanii bora wa kike wa muziki pamoja na Lady Jay Dee, Mwasiti, Shaa na malkia wa mipasho, Khadija Kopa. Wasanii haohao pia wameteuliwa kwania tuzo ya mwanamuziki bora wa kike.

Linah pia anawania tuzo ya wimbo bora wa R&B kupitia wimbo wake wa Atatamani ambapo katika kipengele hiki anawania na Belle 9 (We ni wangu), Ben Poul (Nikikupata), Hussein Machozi Feat Maunda Zorro (Hello) na Z- Antol kupitia wimbo wake wa Kisiwa cha Malavidavi.

Kipengele kingine anachowania Linah ni tuzo ya msanii anayechipukia ambapo atapambana na Sam wa Ukweli, Sajna anayetamba na wimbo wake wa Iveta, Bob Junior anayetamba na wimbo wa Oyoyo na Top C anayetamba na wimbo wa Lofa. Pia Linah anawania tuzo ya wimbo bora wa Zouk kupitia wimbo wake wa Bora nikimbie akishindana na Sam wa Ukweli (Sina raha), Top C (Lofa), Barnaba (Nabembelezwa) na  Amini (Robo saa).

Kwa upande wa wimbo bora wa taarab, nyimbo zinazowania tuzo ni My Valentine (Jahazi), Top In Town (Khadija Kopa), Acheni Kuniandama (Isha Ramadhani ‘Mashauzi’), Langu Rohoni (Jahazi) na mama nile radhi wa Isha Mashauzi.

Aidha wimbo bora wa Kiswahili (bendi) zitakazowania tuzo ni Shika ushikapo (Mapacha watatu), Laptop (Extra bongo), Kauli, Mapenzi hayana kiapo (Twanga Pepeta) na Pongezi kwa wanandoa (Acudo) huku kwa upande wa repa bora wa mwaka wakishindanishwa Ferguson wa Extra Bongo, Khalid Chokoraa wa mapacha watatu, Totoo za bingwa wa Acudo na Kitokololo wa FC Academia.

Kwa mujibu wa Kavishe, kura zitaanza kupigwa Machi mosi mpaka Machi 22 kabla ya kufanyika kwa fainali za tuzo hizo Machi 26.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW