Habari

Watoto 20 wafa kwa ajali ya gari SA

By  | 

Watoto 20 wamefariki katika ajali ya barabarani katika mkoa wa Mpumalunga nchini Afrika Kusini kaskazini mwa mji mkuu wa Pretoria.

Basi hilo likiwa umeungua moto na lori la mizigo

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, basi dogo la wanafunzi walilokuwa wakisafiria liligongana na lori na kulipuka.

Russel Meiring ,ambaye ni msemaji wa shirika la matibabu ya dharura ER24, ameambia Reuters kwamba watoto 20 walikuwa ndani ya basi hilo wakati lilipogongana na lori la kubeba mizigo.

Chapisho la awali ambalo lilithibitisha watoto 13 kufariki ilionyesha eneo la ajali hilo.

Panyaza Lesufi, afisa anayehusika na elimu katika mkoa wa Gauteng amesema kuwa ni ‘siku nyeusi’.

Haijajulikani ni nini haswa kiini cha ajali hiyo, lakini picha zinaonyesha basi hilo limeungua kabisa.

Baada ya moto kuzimwa, maafisa wa matibabu walipata watoto 13 wakiwa wamekwama ndani ya gari hilo.

“Hawakuweza kunusurika na wakatajwa kuwa walifariki papo hapo,” taarifa hiyo ilisema.

ER24 na idara ya elimu katika mkoa wa Gauteng zimethibitisha kwamba watu 20 walifariki.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments