Habari

Watoto wa mbowe pamoja na Mh. Lowasa, Zitto Kabwe, Lema watinga mahakamani, Rufaa ya kesi ya Mbowe na Matiko yapigwa tarehe (+ Video)

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mhazini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko leo Jumatatu wamerejeshwa gerezani baada ya Mahakama ya Rufaa kusema itatoa uamuzi wa rufani iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi yao tarehe na siku itakayopangwa.

Mahakama hiyo ya rufaa imewataka mawakili wa serikali waeleze kwanini walipeleka shauri la kupinga dhamana mahakamani hapo badala ya kutoa muda kwa mahakama kuu ili waweze kusikilizwa.

Hata hivyoo jaji wa kesi hiyo ameahirisha shauri hilo mpaka kesho ili aweze kutoa maamuzi ya awali ya dhamana ya Mh mbowe na Mbunge Esther Matiko.

Huku kesi hiyo ikihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa, mwenyekiri wa ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe, Lema na wengine wengi bila kuwasahu watoto wake waliofika mahakamani hapo kusikiza shauri hilo linalomkabili baba yao.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents