Habari

Watoto wa shule za msingi wawapa mimba wa sekondari

WANAFUNZI wanne wa shule za msingi katika Wilaya ya Mtwara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara kwa tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi wenzao wa kike wa shule za sekondari wilayani hapa.

Hassan Simba, Mtwara

 

WANAFUNZI wanne wa shule za msingi katika Wilaya ya Mtwara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara kwa tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi wenzao wa kike wa shule za sekondari wilayani hapa.

 

Katika kesi ya kwanza mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Dihimba, Mabruki Hamis (17) alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mtwara, Paulidindo Ntumo akituhumiwa kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Dihimba, Mwajuma Salumu (19).

 

Ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Nurudin kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Novemba mwaka jana. Mtuhumiwa alikana mashitaka na kesi hiyo inaendelea kusikilizwa.

 

Katika kesi nyingine, mwanafunzi wa darasa la tano wa Shule ya Msingi Mnaida Daruweshi Hamis (14) amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mtwara, Ramadhan Rugemarila akituhumiwa kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mnaida, Mwanahamisi Mussa (16). Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Sendoyeka alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari hadi Juni mwaka huu.

 

Mwingine aliyefikishwa mbele ya mahakama hiyo ni mwanafunzi Sadick Shea (14) anayetuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi mwenzie, Zuhura Salehe (18) wote wa Shule ya Msingi Tangazo iliyopo Halmashauri ya Mtwara Vijijini. Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili mwaka jana.

 

Pia mahakama hiyo inaendelea kusikiliza kesi ya mwanafunzi mwingine wa darasa la saba Shule ya Msingi Mnima, Mudhihiri Salum (16) akidaiwa kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mnima, Zuhura Said (15). Watuhumiwa wote wamekana mashitaka yao na wako nje kwa dhamana na kesi zao zinaendelea kusikilizwa.

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents