Afya

Watoto wanaotumia vinywaji vya kuongeza nguvu ‘Energy’ wapo hatarini kutumia Cocaine

Kama mzazi au mlezi huwa watoto wako unawanunulia vinywaji vya kuongeza nguvu ‘Energy’ basi halitakuja kuwa jambo la kushangaza kuona baadae ukubwani wakitumia madawa ya kulevya kama Cocaine hii ni kutokana na tafiti zilizofanywa.

Tokeo la picha la children drinks energy

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Dr Amelia Arria kutoka Chuo kikuu cha Maryland nchini Marekani zimeeleza kuwa watoto waliochini ya umri wa miaka 16 wanaotumia vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy) asilimia kubwa wengi wao baadae ukubwani hujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na ulevi wa kupindukia.

Kwenye utafiti huo pia umeonesha kuwa kutokana na msisimko wanaoupata wanapokunjwa vinywaji hivyo watoto wengi wakishafikisha umri wa miaka 25 hujiingiza kwenye matumizi ya pombe.

Mpaka sasa watafiti wengi duniani wameviingiza vinyaji vya kuongeza nguvu (Energy Drink) kwenye orodha ya vinywaji haramu kutokana na uwingi wa Caffein huku wakifeli kuelezea uhusiano wa Caffein na madawa ya kulevya kama Cocaine.

Hata hivyo vinywaji vya kuongeza nguvu bado havijatambuliwa na mashirika makubwa yanayohusika na vyakula na madawa kama (Food and Drug Administaration) hii ni kutokana na kificho cha kiwango cha Caffeine kinachowekwa kwenye vinywaji hivyo kupitiliza.

Kwenye utafiti huo alitumia vijana 1,099 watumiaji wa vinywaji hivyo waliochini ya umri wa miaka 21 na baada ya miaka mitano baadae asilimia 94% walikuwa watumiaji wa pombe kupindukia na mihadarati.

Kwa nchi za kiafrika kutokana na tamaduni za kutokusoma maelezo ya bidhaa kabla ya kuitumia, utumiaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy) umeongezeka kwa asilimia 45 kati ya mwaka 2010/17 kutoka asilimia 19 mwaka 2009.

Bara la Afrika linakuwa bara la kwanza duniani kwa utumiaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy) kwa mwaka 2016/17 ikifuatiwa na bara la Asia na Amerika ya Kaskazini kwa mujibu wa mtandao wa Fast Moving.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents