Burudani

Watu 100 kufuturishwa kila siku na Candy and Candy

Kampuni ya Candy and Candy inayojihusiha na mambo mbali mbali katika sekta ya burudani ikiwemo kutengeneza filamu na kusimamia wasanii inatarajia kuja kivingine katika msimu huu wa Ramadhani.

Kampuni hiyo itatumia mfumo wa mpya uliouanzisha wa kiteknolojia uitwao ‘Nikohub’ kwa ajili ya kufuturisha watu 100 kila siku kwa muda wa siku kumi mfululizo.

Ili uweze kupata nafasi ya kushiriki Futari hiyo utataiwa ku-download app ya ‘Nikohub’ kwenye Play Store ya simu yako.

“Jiunge ili tuweze kukuona kwenye mfumo wetu wa app ya Nikohub, iliuingie kwenye list ya watu 100 watakao kula futari leo, ukifanikiwaku-downloda tu tumia SMS au piga 0765802457 ili basi tukuelekeze sehemu ya kwenda kula futari maeneo ya huko ulikoni bure,” amesema Joe Kariuki.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents