Habari

Watu 137 waliopoteza ndugu MV Nyerere waanza kupokea milioni 1 kwa kila mmoja

Watu 137 waliopoteza ndugu katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere wameanza kupokea mkono wa pole wa Sh1 milioni kwa kila marehemu aliyetambuliwa na kuchukuliwa kwa mazishi.

Awali, ndugu hao walishakabidhiwa mkono wa pole wa Sh500, 000 kwa kila mwili uliotambuliwa.

Wameanza kupokea fedha hizo kuanzia leo asubuhi Jumanne Septemba 25, 2018.

Nyongeza ya Sh1 milioni ni agizo la Rais John Magufuli alilolitoa jana akitaka fedha zote za rambirambi zinazochangwa na mashirika, taasisi, makampuni na watu binafsi kutumika kupewa wafiwa.

Fedha hizo pia zitatumika kujenga uzio na makaburi wanakozikwa baadhi ya waliokufa kwenye ajali hiyo iliyotokea Alhamisi Septemba 20, 2018.

Maiti iliyozikwa kwa kukosa ndugu yatambulika Ukerewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents