Habari

Watu 18 wafariki kwa Ebola

Wiki liyopita shirika la Afya duniani (WHO)lilitangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika nchi Jamuhuri ya democrasia ya congo(DRC).

Majaribio ya chanjo ya ugonjwa wa Ebola yamebainika kuwa yana uwezo na nguvu zaidi dhidi ya virusi vya ugonjwa huo hatari. Licha ya kuwepo kwa majaribio ya chanjo hiyo katika nchi za Afrika ya kati, bado ugonjwa huu umeendelea kuteketeza maisha ya watu.Kwa mujibu wa WHO mapema Jana,wameripoti jumla ya watu 18 kufariki katika nchi hiyo ya DRC.

Kwa mujbu wa takwimu za WHO zimeripoti kuwa eneo hilo la DRC lililokumbwa na ugonjwa huo wa Ebola ni eneo hatari kwa sasa barani Afrika.Waliokufa kwa ugonjwa huo ni pamoja na mwanamume wa umri wa miaka 39 aliyetajwa kuwa pamoja na watu wawili ambao walikuwa wamekaribiana nae.

Zaidi ya watu 11,000 wanaripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika tangu mwaka 2014 na 2015 hasa nchini za Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents