Burudani

Watu 19 wafariki dunia kwenye show ya Ariana Grande Uingereza

Jumatatu hii show ya ziara ya Ariana Grande ya “Dangerous Woman” imeingia dosari.

Show hiyo ambayo ilikuwa inafanyika katika ukumbi wa Manchester Arena mjini Manchester, Uingereza ilivunjika baada ya kutokea mlipuko na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 50 kujeruhiwa.

Ukumbi huo una uwezo wa kuchukua watu 21,000 na barabara zake zinaungana kituo cha treni cha Victoria katikati mwa mji. Grande kupitia mtandao wa Twitter ameomnyesha kuhuzunishwa na tukio hilo kwa kuandika, “broken. from the bottom of my heart, i am so so sorry. i don’t have words.”

Naye Nicki Minaj ambaye ni mmoja ya watu wakaribu wa muimbaji huyo wa Pop, kupitia mtandao huo amempa pole kutokana na tukio hilo kwa kuandika, “My heart hurts for my sister, Ariana & every family affected by this tragic event in the U.K. Innocent lives lost. I’m so sorry to hear this.”

Wakati huo huo waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May ametaja tukio hilo kama kitendo cha kigaidi ambapo ni mara ya kwanza linatokea tangu lile la mwezi Julai mwaka 2005 ambapo zaidi ya watu 50 walifariki dunia mjini London.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents