Habari

Watu 25 wafariki dunia kwa moto Ureno

Watu 25 wamefariki dunia na wengine takriban 20 wamejeruhiwa kutokana na moto mkubwa uliozuka katika msitu uliopo katikati mwa nchi ya Ureno.

Kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo imedai, watu wengi walifariki wakati walipokuwa wakijaribu kuyakimbia maeneo ya Pedrogao Grande yaliyopo Kusini Mashariki mwa mji wa Coimbra.

Naye waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, João Gomes amewaambia waandishi habari kuwa watu 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, pale walipokabiliwa na moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande katika barabara inayounganisha miji ya Figueiro dos Vinhos na Castanheira de Pera.

Wakati huo huo waziri mkuu António Luís Santos da Costa, amesema hilo ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents