Habari

Watu 30 wafa maji DRC huku wengine zaidi ya 300 hawajulikani walipo, kufuatia ajali mbaya ya boti kutokea eneo la Inongo Magjaribi mwa nchi hiyo

Usafiri wa majini umeendelea kuwa jinamizi kwa wasifiri nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya ajali ya boti kugharumu maisha ya watu 30, huku wengine zaidi ya 300 hawajulikani walipo katika eneo la Inongo Magjaribi mwa nchi hiyo

BOTI

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Ajali hiyo ambayo ni mwendelezo wa majanga ya majini nchini DRC imetokea usiku wa Jumamosi kwenye ziwa Mai-Ndombe, na bado mamia ya wale walioabiri boti hiyo hawajapatikana mpaka sasa.

“Mapaka sasa tumeshapata maiti 30, wanawake 12, watoto 11 na wanaume saba,” Meya wa Inongo Simon Wemba ameliambia shirika la habari la kimataifa la AFP.

“Idadi hiyo ya vifo ni ya muda huu, na yaweza kubadilika muda wowote,” Wemba amesisitiza, akiongeza kuwa ni vigumu kujua kwa hakika boti hiyo ilikuwa imebeba abiria wangapi na yawezekana ilikuwa imesheheni wahamiaji haramu.

Wemba amesema kuwa waliokolewa kwenye ajali hiyo ni watu 183, chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni hali mbaya ya hewa.

Boti hiyo pia inaaminika kuwa ilipakiza idadi kubwa ya walimu ambao walikuwa wanaelekea kupokea mishahara yao.

Janga la majini DRC

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni mwezi mmoja tu toka watu 167 walipofariki kwenye ajali mbili za majini kwenye nchi hiyo. Ajali hizo zilimlazimu rais wa DRC Felix Tshisekedi kuamrisha kuwa abiria wote wa vyombo vya majini nchini humo wavalishwe maboya muda wote wa safari.

DRC ambayo ndiyo nchi kubwa zaidi barani Afrika, inategemea mito na maziwa kama njia za usafiri wa watu na mizigo na kuunganisha maeneo kadhaa ya nchi hiyo ambayo ni vigumu kufikika kupitia barabara.

boti la kifahari

Hata hivyo, usafiri huo umekuwa wa hatari kwa usalama, na licha ya serikali kuchukua hatua mbadala kutafuta ufumbuzi katika suala hilo bado hali si swari.

Ajali nyingi husababishwa na matatizo ya kiufundi ya vyombo vya majini pamoja kujaza watu na kupita kipimo.

Idadi ya vifo huwa kubwa sababu abiria hawavai maboya ya uokozi, lakini pia raia wengi wa nchi hiyo hawajui kuogelea.

Watu 27 walipoteza maisha baada ya bot yao kuzama Septemba mwaka jana, 26 mwezi Julai, 50 mwezi Mei na 40 mwezi Aprili wakiwa njiani kukimbia mapigano mashariki mwa nchi hiyo.

Majanga hayo ya majini pia yanatokana na serikali ya nchi hiyo iliyopo mji mkuu wa Kinshasa kushindwa kusimamia vizuri utekelezwaji wa sheria kutikana na maeneo mengi yenye mito na maziwa kuwa mbali na nchi hiyo kukumba wa mapigano.

Majanga Afrika Mashariki

Jumanne wiki iliyopita ilitimia miaka 23 tangu kisa cha ajali ambayo inatajwa kuwa mbaya zaidi katika karne kutokea barani Afrika katika ziwa victoria nchini Tanzania.

Ni janga ambalo lilisababisha idadi kubwa ya watu wapatao 1000 kupoteza maisha baada ya meli ya Mv Bukoba kuzama.

 

Kwa miaka yote hiyo Tanzania imeendelea kukumbwa na majanga makubwa na madogo ya majini.

MV Nyerere

Mwaka jana, Septemba 2018 jumla ya watu 224 walifariki na watu wengine 41 wakiokolewa wakiwa hai katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Mwaka 2011 na 2012 watu zaidi ya 250 walipoteza maisha kwenye bahari ya Hindi baada ya kuzama kwa meli za Mv Spice Islander na Mv Skagit.

Jumatatu iliyopita, Mei 20,2019 ajali ya majini ilitokea na kuua watu 16 huku wengine wakiwa hawajulikani walipo nchini Uganda.

Boti iliyokuwa imebeba wacheza mpira 50 wakiwa na mashabiki wao magharibi mwa Uganda.

Mwaka 2016 , wachezaji 30 wakiwa na mashabiki wao walizama katika ziwa Albert na watu 20 walifariki.

Uganda

Mwaka 2018 watu 29 walifariki kufuatia ajali ya boti iliyotokea ziwa Victoria, nchini Uganda.

Boti hiyo iliyokuwa na watu zaidi ya 90 waliokuwa wanaelekea kwenye sherehe, ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono.

Mwaka 2014, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa takriban watu 98, wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wanasafiria kuzama katika Ziwa Albert Magharibi mwa Uganda.

Boti iliyozama ilikua imebeba zaidi ya wakimbizi 100.

Aliyekuwa anaendesha boti hiyo alikamatwa na jeshi la polisi na inadaiwa kuwa alikua mlevi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents