Watu 40 mbaroni kwa tuhuma za kuwakata kwa mapanga wanachama wa CCM, Pemba (+Video)

Watu zaidi ya 40 wamekamatwa na jeshi la polisi visiwani Pemba kwa kuwajeruhi baadhi ya wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wanatoka msikitini.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, akizungumza wakati wa ziara yake mkoani pwani amesema  wameshakamatwa watu zaidi ya 40 na tiyari ulinzi umeimarishwa.

Wahalifu waliokata mapanga baadhi ya  wakereketwa wa CCM, wamewajeruhi walikuwa wanatoka msikitini lakini Watu zaidi ya 40 na wamekamatwa nachotaka kusema wale wanajaribu toka jana tumeimarisha sana ulinzi pale

Aidha IGP Sirro, ameongelea kuhusiana na baadhi ya watu kudai wanaowasikiliza wataingia barabarani kwa kusema kuwa watanzania sasa hivi wanauelewa hivyo wanavyokwenda kwenye mikutano ya kampeni wanasikiliza sera na si sikuhamasishwa kuingia barabarani

Nimekuwa nikisikia watu wengine wanasema hawa watu wote wanaonisikiliza wataingia barabarani niseme wale watu wote wanaokwenda kwenye ule mkutano wanaenda kusikiliza sera wala hawaendi kwa ajili ya kuandaliwa kuingia barabarani” amesema IGP Sirro.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW