Habari

Watu wa Lugola wanaodaiwa kupewa Laptops na posho za dola 800 kila kikao waendelea kuhojiwa Dodoma – Video

Watu wa Lugola wanaodaiwa kupewa Laptops na posho za dola 800 kila kikao waendelea kuhojiwa Dodoma - Video

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani Dodoma, imeendelea kuwahoji waliokuwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji wa makubaliano, yaliyosainiwa Agosti 22, 2019, kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kampuni ya Rom Solution Co LTD.

Viongozi sita wa Jeshi la Zimamoto wakiwa katika ofisi za TAKUKURU Dodoma.

Wajumbe hao ni wale wanaodaiwa kupewa laptops na posho za vikao na safari kwa kila kikao Dolla 800 za Kimarekani na kampuni hiyo, wakati wakiwa wanakutana katika vikao vyao vya majadiliano.

Wajumbe hao wamefika kwenye mahojiano wakiwa na laptops walizopewa na kampuni hiyo, ambao ni Kamishna wa Zimamoto Baraka Semwanza, Naibu Kamishna Zimamoto Fikiri Salla, Naibu Kamishna Zimamoto Lusekelo Chachula, huku wengine wakiwa ni Naibu Kamishna Ully Mburuko, Mchumi wa Jeshi la Zimamoto Boniface Kipomela na Mchumi wa Zimamoto Felis Mshana.

Hatua hii inakuja ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, aliyewaagiza TAKUKURU kuwa wahakikishe wale wote waliohusika na mkataba hewa wa Trilioni 1 ambao haukuwa umepitishwa na Bunge, wanahojiwa akiwemo aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

Video Credits by Clouds media.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents