Habari

Watu waliofariki katika maporomoko Congo wafikia 200

Idadi ya watu ambao wameuawa kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, huenda ikapanda hadi kufikia watu 200, maafisa wamesema.

Watu ambao walikufa ni kutoka jamii ya wafugaji katika ziwa Albert.

Maafisa wanasema kuwa idadi hiyo ni kutokana na idadi ya familia zilizofukiwa baada ya mvua kubwa kusababisha sehemu za mlima ulio karibu kuporomoka.

Matumaini ya kuwapata manusura yamedidimia wakati waokoaji wakiwa hawana njia za kuondoa mawe makubwa.

“Kuna watu wengine zaidi waliofukiwa ambao hatuna uwezo wa kuwakoa,” naibu gavana wa mkoa wa Ituri aliliambia shirika la Reuters.

Sehemu nyingi za magharibi na kati kati mwa Afrika zinakubwa na maporomoko ya ardhi kwa sababu miti imekatwa sana na jamii zimesongamana kwenye maeneo yaliyo chini ya milima.

Mashariki mwa Congo ni eneo ambalo pia hukumbwa na mitetemeko ya ardhi.

Zaidi ya watu 400 wameuawa huku 600 wakiwa hawajulikani waliko baada ya janga kama hilo kuikumba Sierra Leone.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents