Habari

Watu waliovalia maski wadaiwa kuvamia nyumba ya Beckham,wakitaka kuiba huku yeye akiwa Australia na mke wake

Polisi wathibitisha kutokea kwa tukio hilo

Aliyekuwa mchezaji wa klabu tatu kubwa duniani ambazo ni Manchester United, Real Madrid PSG pamoja na timu ya taifa ya Uingereza David Beckham apatwa na janga la kuvamiwa na Wanyang’anyi kwa kuvunja sehemu ya nyumba yake inayodaiwa kuwa na thamani ya Euro milioni 6.

Wanyang’anyi hao waliokuwa wamevalia Balaclava (Mask za kofia) inadaiwa walijaribu kuvunja ndani ya nyumba hiyo  ya Victoria na David Beckham huko Great Tew, Oxfordshire sehemu ilipo nyumba hiyo nchini Uingereza wiki iliyopita.

Wanyang’anyi hao wakiwa watatu walidaiwa kupada ngazi kuelekea ulipo ukuta wa nyumba hiyo karibu na kwenye dirisha la ghorofa ya kwanza, kabla ya kufukuzwa na wageni pamoja na wamiliki waliokuwa karibu na klabu ya Soho Farmhouse.

Posh na Becks wanaaminika kuwa walikuwa wameenda kutembea katika taifa la Australia kwa wakati huo, wakati wakiongea na kuliambia jarida la Mirror Online baada ya kuweka wazi hilo.

Mirror walisema kuwa Beckham na mke wake walisema “Wao ni wazi wameshtushwa na tukio hilo na wanatarajia na kuamini kuwa  hao wavamizi hawakupata chochote na wamezuiliwa kufanya hivyo tena”

Mwandishi wa pili aliiambia Daily Mail kuwa: “Beckham anachukizwa na ni ukweli kwamba anapaswa kuwa na Ulinzi na usalama wa juu sana na wa karibu sana karibu naye lakini angependa kuwa wa kawaida na kuishi maisha ya kawaida yeye kipaumbele chake cha kwanza ni kumlinda mke wake, watoto wake pamoja na familia yake kiujumla”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents