Habari

Watu wanaokebehi Ripoti ya Bunge kuhusu Richmond wapewa onyo

WATU wanajitokeza hivi karibunu kuhoji na kukebehi maamuzi ya Bunge yaliyotokana na mapendekezo ya Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza kashfa ya zabuni ya Umeme wa dharura iliyopewa kampuni ya Richmond Development, wanaweza kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Na Muhibu Said

 

WATU wanajitokeza hivi karibunu kuhoji na kukebehi maamuzi ya Bunge yaliyotokana na mapendekezo ya Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza kashfa ya zabuni ya Umeme wa dharura iliyopewa kampuni ya Richmond Development, wanaweza kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

 

 

 

Onyo hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Juma Suleiman Nh’unga, alipozungumza na mwandishi wa gazeti hili jana.

 

 

 

Nh’unga ambaye ni Mbunge wa Dole (CCM) alisema Ofisi ya Bunge iko macho na watu hao na kwamba, inafuatilia na kufanyia kazi vitendo wanavyofanya.

 

 

 

“Kama wataonekana wamekiuka, wataitwa, watahojiwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge,” alisema Nh’unga.

 

 

 

Onyo hilo limetolewa na kamati hiyo baada ya kutakiwa kueleza msimamo wa Bunge kuhusiana na baadhi ya watu kuhoji maambuzi ya Bunge ya ripoti na mapendekezo hayo kupitia njia mbalimbali, ikiwamo mikutano na waandishi wa habari na vipeperushi.

 

 

 

Naye Mnbunge Lucas Selelii ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati Teuleya Bunge iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyemba, alisema kitendo cha kuhoji na kukebehi ripoti na mapendekezo ya kamati hiyo nje ya vikao vya Bunge ni cha kulidhalilisha Bunge na kamwe hakiwezi kukubalika.

 

 

 

“Wanaokebehi na kuhoji ripoti na mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge, wajiandae kuitwa na kuhojiwa na Bunge. Hatuwezi kukubali Bunge lidhalilishwe,” alisema Selelii.

 

 

 

Selelii ambaye ni Mbunge wa Nzega (CCM) alisema hawakubaliani na vitendo hivyo kwa kuwa Bunge lilitoa mapendekezo yake ili serikali iyafanyie kazi na kwamba, halikufanya hivyo ili kutoa fursa kwa watu kuitisha mikutano ya waandishi wa habari kuhoji na kukebehi vitu hivyo.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents