Habari

Watu wanaotekwa hawatekwi na watu waliopo mbinguni – M/Kiti UVCCM

Mwenyekiti wa wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Kheri James amesema kuwa watu wanaotekwa hawatekwi na watu waliopo mbinguni hivyo watekaji wataonekana tu.

Kheri ameyazungumza hayo katika Kipindi cha Kingaangoni kinachorushwa na EATV amesema kuwa kwenye suala la utekaji hilo ni jukumu la msingi na si kujitenga nalo

“Watu wanaotekwa hawatekwi na watu waliopo mbinguni, kwenye hili wala tusijitenge tunalo jukumu la msingi,” amesema Kheri James.

“Leo inashangaza mtu anaweza kutekwa inapita wiki au mwezi, mtu hajatekewa London ametekewa Manzese hapo, jamanii turudishe mapenzi na kupendana mwisho wa siku watekaji wataonekana na kufahamika tu”.

Kumekuwa na watu kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana ambao mpaka leo hawajafahamika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents