Habari

Watu wanauliza: Bob Haisa kawa chizi kweli?

Hii picha imesambaa kwenye mtandao wa Facebook ikimwonesha Bob Haisa akiwa kama chizi na kuzua maswali mengi kama ni kweli ama ni harakati tu za kufanya sanaa.

Picha hiyo imewekwa na mtangazaji wa Kiss FM, D7.

Baada ya kuona kuwa kila mmoja anazungumza lake, Bongo5 imemtafuta Bob Haisa ambaye baada kucheka sana aliposikia jinsi watu wanavyoizungumzia picha hiyo, amesema hiyo picha ni ya video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Wa Kukaya’

“Safari hii sikupenda kuweka madancers kwenye video, nimeamua kuigiza mwenyewe kama Pedeshee, Choka Mbaya nk.

Amesema video hiyo bado ipo kwenye hatua za mwisho kumalizika ili itoke.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents