Tupo Nawe

Watu wapanga foleni nyumbani kwa Chris Brown kununua nguo na viatu alivyokwisha vitumia – Video

Watu wapanga foleni nyumbani kwa Chris Brown kununua nguo na viatu alivyokwisha vitumia - Video

Mkali wa R&B Duniani @chrisbrownofficial alikuwa mnada wa uuzwaji bidhaa zake ambazo tayari ameshazitumia au kuzivaa hasa nguo na viatu nyumbani kwake mnada unaotarajiwa kuchukua mbili na jana siku ya Jumatano nyumbani kwake Los Angeles mamia ya mashabiki zake walijazana wakiwemo walanguzi na wanaotafuta biashara pamoja na bidhaa za kuuza wakisubiri masaa mengi kujaribu kupata bidhaa kutoka kwa mwimbaji huyo ili wakawauzie watu wengine au wengine wakavae kabisa.

Brown alituma vipeperushi kwenye akaunti yake ya Instagram na Twitter Jumanne usiku ambayo ilijumuisha anwani ya jumba lake lililopo katika kitongoji cha Tarzana kwenye Bonde la San Fernando Los Angeles Marekani akiwajulisha watu watakaovutiwa kwenda kupata bidhaa au hata kununua nguo za kuvaa kuhakikisha wanafika nyumbani kwake, na watu mbalimbali wakiwemo mashabiki zake waliitikia wito huo.

ujumbe ulisomeka “DA CRIB … tukio la siku 2” akiweka pamoja na emoji ya moyo.

Na hili ndio balaa lililoyokea nyumbani kwake siku ya jana tarehe 6/11/2019.
:
Brown, ambaye mara nyingi anajulikana na jina lake la utani Breezy, alililipata jukwaani mnamo mwaka 2005,na ikumbukwe alishinda tuzo ya Grammy mnamo 2011 kwa albam bora ya R&B na anabaki kuwa major hitmaker mkubwa. Albamu yake mpya “Indigo” ilikwenda mpaka Na. 1 wakati ilitolewa mnamo Juni, mwaka 2-019 huku wimbo wake wa “No Guidance” featuring Drake and he’s ukiwa nominated for a pair of American Music Awards

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW