Habari

Watu wasio pungua 11 wafariki dunia kwa kupigwa risasi huko pwani ya Mexico.

Kulikuwa na mvutano baina ya wakazi na wajumbe wa polisi wa mitaa, waliochaguliwa na jumuiya nje ya jiji la Acapulco.
Vita vya bunduki vilifanyika katika jumuiya ya kilimo ya La Concepcion, baada ya kijana mmoja kukamatwa kwa uovu wakati wa mikutano ya mji mapema Jumapili asubuhi.Wakazi nane waliuawa katika mabadilishano hiyo.

Baada ya askari wa Jeshi la polisi la serikali kufika eneo hilo , wajumbe watatu wa polisi wa jamii walipigwa risasi baada ya kuwapinga, viongozi walisema.
Polisi wengine 30 wa mtaa, ambao walikuwa wameidhinishwa na viongozi wa serikali kufanya kazi katika mji mdogo, walikamatwa katika operesheni.

Acapulco ni jiji kubwa zaidi katika jimbo la kusini la Guerrerona.
Vurugu katika jimbo hilo pia limekuwa likisababishwa na vita dhidi ya usambazaji wa dawa za kulevya kama cocaine na methamphetamine.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents