Habari

Watu wawili mbaroni kwa kuchoma nyumba 14

Jeshi la polisi mkoani Kagera, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba 14 wilayani Muleba mkoani humo.

Kamada wa Polisi mkoani humo, Augustino Ollomi amesema polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa mmoja ambaye ana sadikiwa kutoroka wakati watuhumiwa wengine walipo kamatwa.

Kamanda Ollomi aliwataja watuhumiwa kuwa ni Angela Kalisti (36) pamoja na Badru Daniel ambaye uraia wake umeonekana ukiwa na utata.

“Huyu ni mshubi alivyotuambia lakini tumebaini kuwa huyu ni Mrundi, kahifadhiwa pale hatujui ni kwa madhumuni gani alitoka wapi anafanya nini pale hakuna mtu anaelewa, kuna mtuhumiwa mwingine alitoroka jana jitihada za kumtafuta bado zinaendelea,” alisema Kamanda Ollomi.

“Hatuwezi kumficha kwasababu ni mtu ambae tuna mtafuta na tutatumia mbinu zote za kipolisi mpaka tumpate uhalifu alioufanya ni mkubwa anaitwa Shakiru Mohamed(42) yeye ni Muhaya na ni mkazi wa kijiji Bugasha pale ambapo matukio kama haya yanatokea.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents