Habari

Watu zaidi ya 50 wauawa Uganda, mfalme wa Rwenzururu atiwa mbaroni

Watu zaidi ya 50 wamefariki dunia kutokana na mapigano yaliyozuka kati ya maafisa wa usalama wa nchi ya Uganda dhidi ya walinzi wa mfalme Charles Wesley Mumbere maarufu kutoka himaya ya Rwenzururu ambao wanataka kujitenga katika jimbo la magharibi la Rwenzori.

589188a7-daad-4ea5-8326-03fae8c8e49c_w610_r1_s

Msemaji wa jeshi la polisi wa Uganda, Felix Kaweesi amesema maafisa 13 wa polisi na wapiganaji 41 wa mfalme huyo waliuliwa katika mapigano makali yalitokea katika wilaya ya Kasese wakati wanamgambo walipowashambulia polisi waliokuwa wanapiga doria.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Rais Yoweri Museveni aliwahi kumpigia simu mfalme huyo kuvunja kundi la walinzi wake kabla ya kukamatwa na maafisa hao wa polisi wa nchi hiyo. Mfalme Mumbere amekanusha kuhusika kwenye mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi yaliyowahi kutokea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents