Technology

Watumiaji wa iPhone sasa wataweza kutuma ujumbe wa WhatsApp hata kama simu isipokuwa na internet

By  | 

Siku za kusubiri uwe internet ili uweze kutuma ujumbe kwenye WhatsApp zinaelekea ukingoni kwa watumiaji wa simu za iPhone.

Feature mpya itawawezesha watumiaji wa simu hizo za kishua (iPhone) kutuma ujumbe wa WhatsApp wakiwa offline. Ujumbe huo utasubirishwa baada ya kuandikwa na kutumwa pindi simu inapopata data. Watumiaji wa simu hizo wanaotaka kutumia feature hiyo wanaweza kufanya hivyo kwa kuweka version mpya WhatsApp (2.17.1) kwenye simu zao.

Kwa watumiaji wa simu za Android wamekuwa wakiweza kufanya hivi tangu kitambo. Watumiaji wa iPhone walikuwa hawawezi kutuma ujumbe bila kuwa na connection. Awali, kitufe cha kutuma kilikuwa hakiwezi kufanya kazi kwenye simu ya iPhone hadi ikiwa na internet.

Hiyo ni update ya kawaida kabisa, lakini yenye umuhimu mkubwa kwa watu wenye mambo mengi. Update hiyo itawawezesha pia watumiaji wa mtandao huo kutuma picha 30 kwa mpigo, tofauti na zamani ambapo waliweza kutuma picha 10 tu.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments