Technology

Watumiaji wa iPhone wanaopenda kutuma sauti na video kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na WhatsApp wapatwa na pigo

Kampuni ya Apple imekuja na mpango wa kudhibiti matumizi ya sauti na video kwenye Apps za Facebook na WhatsApp kwenye simu zao za iPhone ili kuboresha na kulinda faragha za watumiaji wa simu hizo.

Apple wamesema wanakusudia kufanya mabadiliko kwenye simu zinazuruhusu kusafirisha sauti na video kwa kutumia Internet yaani “Voice Over internet protocol (VoIP)” ili kulinda faragha za watumiaji na usalama.

Katika mabadiliko hayo, Mfumo endeshaji wa iOS hautaruhusu Apps zisizotumika kuendelea kufanya kazi nyuma kiholela kwenye simu zao za iPhone. Apps kama vile Facebook, WhatsApp, Skype na zingine zinazotegemea teknolojia ya VoIP, Zitaathirika zaidi na uamuzi huo.

Lengo kubwa la uamuzi huo wa Apple ni kulinda faragha ya watumiaji wa simu za iPhone. Imeelezwa kuwa Apps hizo zikiwa zinafanya kazi huwa  zinakusanya data kuhusu mtumiaji wa simu husika.

Mabadiliko hayo yataanza kufanya kazi kwenye toleo jipya la iOS 13, Ambalo linatarajiwa kutoka rasmi mwezi Septemba mwaka huu.

Kwa upande mwingine, Wamiliki wa Apps hizo wamepewa ‘deadline’ hadi mwezi Aprili mwaka 2020, kuhakikisha kuwa Apps zao zinafuata utaratibu  na kanuni mpya za Apple ili waweze kufanya kazi vizuri.

Mabadiliko hayo, Yatasababisha baadhi ya jumbe na video zinazoonesha picha chafu, uchochezi, ubaguzi wa rangi na zile zinazoonesha udhalilishaji wa namna yoyote ile kuzuiliwa kutumwa kwa kutumia simu za iPhone.

Chanzo: https://www.gadgetsnow.com/tech-news/apple-has-a-warning-for-facebook-google-and-why-its-good-news-for-users/articleshow/70697481.cms?utm_source=twitter.com&utm_medium=social&utm_campaign=GNWeb

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents