Habari

Watumishi wa Muhimbili waaswa kutojihusisha na rushwa

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendesha mafunzo ya siku mbili ambayo yamelenga kuwakumbusha watumishi wa hospitali hiyo kuzingatia sheria ya kupambana na rushwa mahali pa kazi sambamba na maadili katika utumishi wa umma.


Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Steven Agwanda akitoa mada katika semina ya siku mbili kuhusu rushwa mahali pa kazi kwa watumishi wa umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Watumishi walikumbushwa kutojihusisha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa pamoja na madhara yanayotokana na vitendo hivyo.

Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bw. Steven Agwanda aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kuzingatia maadili kwa sababu makosa mengi ya rushwa yanasababishwa na ukiukwaji wa maadili.

“Kuna uhusiano mkubwa kati ya rushwa na maadili, mtumishi au viongozi hawachukui rushwa kwa sababu hawana hela, hapa tatizo ni ukosefu wa maadili, zikiwamo tamaa ambazo zinasababishwa na watumishi au viongozi,” alisema Agwanda.

Mafunzo hayo ya siku mbili yalifunguliwa na Mkuu wa Idara ya Ajira na Mafunzo,Abdallah Kiwanga na yaliwalenga wakuu wa vitengo na wasimamizi wa wodi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents