Bizzare

Watupwa jela miaka 2 kwa kuua nguruwe kwa kuwapanda mgongoni (+Video)

Vijana wawili nchini Hispania wametupwa jela miaka miwili kwa kosa la kuuwa nguruwe 79 .

Vijana hao wawili DAA na MR wakisikiliza hukumu yao mahakamani jumatatu ya wiki hii. (Picha na Publico -Esp)

Vijana hao waliingia katika shamba moja la nguruwe huko mjini Huércal-Overa, Almeria na kuanza kuruka juu ya migongo ya nguruwe hao kitu ambacho kilisababisha vifo vya nguruwe 79 na wengine 29 kuvunjika.

Kijana wa miaka 19 ambaye jina lake limefupishwa kwa (DAA) kwa sababu za kiusalama alirekodiwa na mwenzake wa miaka 27 wakati akifanya kitendo hicho bila kujua kama anarekodiwa.

Wakati wanajitetea mahakamani walisema hawakujua kitendo hicho kingeweza kupoteza uhai wa nguruwe hao kwani walijua ni mchezo tuu wa utotoni.

Hata hivyo mmiliki wa shamba hilo la nguruwe amesema alishangaa baada ya siku mbili baada ya kutokea kwa tukio hilo, nguruwe wengi kuvunjika miguu na wengine kufariki bila kuelewa chanzo ni nini.

Lakini baada ya mwaka moja mbele alitumiwa meseji na moja ya vijana hao akimpa pole kwa tukio hilo, huku wakimuomba msamaha kwa kukiri kutenda kosa hilo.

Vijana hao wawili  wamesema wakati wa kurekodi mmoja wao DAA hakujua kama anarekodiwa na baadaye baada ya kuoneshwa video alimshauri MR aifute video hiyo.

DAA ambaye ndiye aliyerekodiwa anasema alishasahau kama alishawahi kufanya tukio hilo lakini alipooneshwa video mbele ya mahakama ndipo alipokuja kugundua kuwa ni yeye na kukumbuka tukio lote.

Tulikuwa tunacheza kwenye shamba la nguruwe ndipo nikaanza kuruka juu ya migongo ya nguruwe na kuwakanyanga wengi walikuwa wakipiga kelele lakini sikuogopa. Lakini baadae tukasikia nguruwe wengi wamekufa, tulikuwa wasiri na sikujua chochote kama mwenzangu alirekodi tukio hilo mpaka alipokuja kunionesha mwezi mmoja baadae“,amesema DAA mbele ya mahakama wakati akijitetea jana mjini Almeria.

Hata hivyo DAA na mwenzake MR wanatakiwa kulipa faini ya dola $5,300 kila mmoja na kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kunyanyasa wanyama na kuuwa.

Masharti mengine waliyopewa na mahakama hiyo ni kuwa hawatakiwi kuwa karibu na wanyama kwa muda wa miaka 3 baada ya kutoka jela.

Kesi ya tukio hilo ilianza kusikilizwa mapema mwaka huu baada ya uchunguzi kukamilika lakini tukio lilitokea Januari 26 mwaka 2016 na hukumu imetolewa jumatatu ya wiki hii.

Chanzo – Publico Esp

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents