Shinda na SIM Account

Waumini 26 wafariki dunia kwa kupigwa risasi wakiwa kanisani Marekani

Kuna nini Marekani? Watu 26 wameuawa kwa kupigwa risasi Jumapili hii wakiwa kanisani kwa ajili ya kufanya ibada mjini Texas na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN limeripoti, mtu mmoja ambaye aliingia katika kanisa la First Baptist Church lililopo katika eneo la Sutherland Springs, Wilson, aliwafyatulia risasi waumini ambao walikuwa wakifanya ibada wakati wa majira ya saa tano asubuhi.

Gavana wa mji huo Greg Abbott amethibitisha idadi hiyo ya vifo vya watu walifariki na amesema kuwa tukio hilo ni kubwa na baya zaidi kutokea katika mji wake.

Mkuu wa idara ya usalama wa Texas, Freeman Martin amesema kuwa mtu huyo alianza kufyatua risasi nje ya kanisa hilo na baadae aliendelea kufanya hivyo mpaka ndani ya kanisa.

Hata hivyo polisi walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa amefarika katika gari lake ambalo lilianguka katika eneo la barabara ya Guadalupe wakati akijaribu kutoroka.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, Rais wa Marekani Donald Trump ameandika ujumbe kupitia mtandao wake wa Twitter unaosomeka, “May God be w/ the people of Sutherland Springs, Texas. The FBI & law enforcement are on the scene. I am monitoring the situation from Japan.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW