Habari

Waumini Anglikana wafanya vurugu

KUFUATIA mgogoro wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Kati ya kumtuhumu Askofu wa Kanisa hilo Bw. Godfrey Mhogolo kuwa anatetea ushoga na usagaji,mvutano wa waumini kanisa hilo umeendelea kuwa mzito.

Na Joyce Kassiki ,Dodoma


KUFUATIA mgogoro wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Kati ya kumtuhumu Askofu wa Kanisa hilo Bw. Godfrey Mhogolo kuwa anatetea ushoga na usagaji,mvutano wa waumini kanisa hilo umeendelea kuwa mzito.


Katika hali isiyo ya kawaida waumini hao jana walifanya vurugu nyingine mbele ya viongozi wa Serikali akiwemo Mbunge wa Dodoma mjini Bw. Ephraim Madeje na Katibu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Dkt Akiri Mwita.


Vurugu hizo zilitokea wakati akisubiriwa Askofu Mhogolo kuja kuendesha ibada ya kipaimara katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu lililopo mjini hapa, ambapo waumini wanaompinga askofu huyo hawakutaka Askofu Mhogolo aingie kanisani na kuendesha ibada hiyo kwa kumsubiri katika lango kuu la kanisa hilo.


Japo waumini hao waliweza kupinga na kuhakikisha haingii kanisani uongozi wa kanisa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walimwezesha Askofu Mhogolo kuingia na kuendesha ibada hiyo.


Kama haitoshi kuwepo polisi kanisani hapo, uongozi wa kanisa ulikodisha walinzi wa Kampuni ya Dodoma Security Guard ili ili kukaa mlangoni na kuhakikisha Askofu Mhongolo anaingia bila matatizo.


Ibada hiyo iliendeshwa chini ya ulinzi mkali huku wakiwepo askari kanzu, polisi na Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU).


Baada ya gari la Askofu kupita lango kuu la kanisa wapinzani hao walilifuata hadi lilipokwenda kusimama karibu Ofisi ya Askofu kwa lengo la kumzuia asiteremke lakini aliwahi kushuka.


Baada ya hapo waumini hao walijipanga kwenye mlango wa kuingilia kanisani ili kumzua Ashofu Mhongolo asiingie kanisani.


Hali hiyo iliwafanya wanaomuunga mkono Askofu huyo kuingilia kati na kujikuta wakitwangana ngumi na wanaompinga jambo lililowafanya polisi kuingilia kati.


Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents