Habari

Wauza unga zaidi wanaswa Dar

Kikosi cha kupambana na madawa ya Kulevya nchini kinawashikilia watu sita kwa kupatikana na madawa mbalimbali ya kulevya.

Na Sharon Sauwa, Jijini



Kikosi cha kupambana na madawa ya Kulevya nchini kinawashikilia watu sita kwa kupatikana na madawa mbalimbali ya kulevya.


Kamanda wa Kikosi cha Madawa ya Kulevya nchini, Kamishna Msaidizi Godfrey Nzowa, amesema watu hao walikamatwa katika matukio tofauti.


Akasema katika tukio la kwanza, Lila Hamis Chalufa,35, mkazi wa Kijitonyama A, amedakwa na kete 13 za madawa ya kulevya aina ya Heroine.


Akasema mtuhumiwa huyo, alikamatwa jana saa 12.30 jioni akiwa katika harakati za kuyauza kwa watumiaji.


Kamanda Nzowa akasema katika tukio lingine, watu wawili wamekamatwa na kete 153 na misokoto 16 ya bangi.


Akawataja watuhumiwa hao kuwa ni Juma Kondo almaaruf Kaulana ,32, na Rajab Kondo,39.


Akasema watuhumiwa hao wamekamatwa saa 2.00 asubuhi leo, katika mtaa wa Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa.


Akasema watuhumiwa hao wote ni wauzaji wa madawa hayo Jijini.


Kamanda huyo, akasema watuhumiwa hao pamoja na wengine watatu watafikishwa mahakamani leo.


Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents