Habari

Wavuvi Tanga wadai bangi inawakinga mashetani baharini

BAADHI ya wavuvi mkoani Tanga wamemuomba Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Sirro kutowakamata wavuvi wanaovuta bangi kwa kuwa wanaitumia kama kinga dhidi ya mashetani na vibwengo wanapokuwa baharini wakivua.

Nestory Ngwega, Tanga


BAADHI ya wavuvi mkoani Tanga wamemuomba Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Sirro kutowakamata wavuvi wanaovuta bangi kwa kuwa wanaitumia kama kinga dhidi ya mashetani na vibwengo wanapokuwa baharini wakivua.


Mmoja wa wavuvi hao alitoa maelezo hayo kwa Kamanda Sirro baada ya kukamatwa akiwa katika harakati za kutengeneza misokoto ya bangi iliyokuwa na uzito wa gramu 2.5 ili kuwauzia wenzake.


Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na msako unaoendeshwa na Polisi mkoani humu katika harakati za kukomesha vitendo vya uhalifu, vikiwamo matumizi ya dawa za kulevya.


Mtuhumiwa huyo Hussein Hassan (19) mvuvi wa eneo la ukingo wa Bahari wa Deep Sea, alimueleza Kamanda Sirro kuwa wanavuta wawapo baharini ili kujiepusha na mashetani yanayoweza kuwadhuru.


Alisema hawavuti kufanya uhalifu, hivyo aliomba asamehewe na wao waruhusiwe kuitumia.


“Kamanda mimi sina kosa, natumia bangi kama kinga yangu na wavuvi wenzangu pia wanatumia bangi kwa kusudi hilo hilo na si kwa maana nyingine.


“Wavuvi wengi tu wanatumia na tunauziana wenyewe kwa wenyewe msokoto mmoja Sh 100, hivyo si kitu cha ajabu. Naomba mniachie tu maana hii ndiyo kinga yetu kule baharini,” alidai Hassan.


Hata hivyo, katika maelezo yake alidai bangi hiyo huletewa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Mzee ambaye ni mtoto wa askari Magereza na amekuwa akifanya biashara hiyo kwa siku nyingi.


“Kijana mmoja ndiye anatuletea mzigo anaitwa Mzee, mama yake nasikia ni askari Magereza, lakini simfahamu jina lake. Mbona Kamanda soko la kumwaga tu baharini, lakini jamani sisi hatuna kosa kwani hatumdhuru mtu, bali hii ni kinga tu tunatumia,” alidai mvuvi huyo kijana.


Souce: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents