Wawakilishi wa Pop Idol watupwa kambini

Michuano ya kumtafuta Pop Idol ambayo inawahusisha washiriki wanne kati ya 1000 waliojitokeza kuwania tiketi ya kwenda jiji Nairobi kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania, wamefanikiwa kupata nafasi hiyo na mpaka sasa wako katika maandalizi

Michuano ya kumtafuta Pop Idol ambayo inawahusisha washiriki wanne kati ya 1000 waliojitokeza kuwania tiketi ya kwenda jiji Nairobi kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania, wamefanikiwa kupata nafasi hiyo na mpaka sasa wako katika maandalizi muhimu kwa ajili ya kuyakabili mashindano hayo.



Washiriki wawili wa shindano la Bongo Star Search (BSS), Godfrey Gregory na Leah Moudy, usiku wa juzi walitangazwa kuwa miongoni mwa washindi katika shindano la kusaka waimbaji, mbali ya washiriki hao waliovuta hisia za wengi, wengine wawili watakaoiwakilisha nchi ni Linda Mwakalyelye na Doreen Aurelian ambao wote ni washindi wa Afrika Mashariki – East African Pop Idols.


 


Akizungumza katika hafla ya kuwatangaza washindi hao, iliyofanyika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa Kampuni ya Multichoice, Lucy Kihwele alisema kwamba, ana imani kubwa washindi hao wataiwakilisha nchi vema.


 


Washindi hao watajumuika na washiriki wengine kutoka nchi za Afrika Kusini, Botswana, Burundi, Visiwa vya Comoro, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Reunion, Rwanda, Shelisheli, Somalia, Swaziland, Uganda, Zambia na Zimbabwe.


 


Mshindi wa shindano hilo atapata mkataba wa kurekodi katika Studio za Sony BMG ambayo ni kati ya kampuni kubwa za kurekodi duniani na kuzawadiwa dola za Kimarekani 80,000.


 


Watanzania wametakiwa kuwapigia kura za kuwawezesha kushinda washiriki wote wa Tanzania mara mchuano huo utakapoanza Mei, mwaka huu na kurushwa na M-Net.



Kampuni ya simu za mkononi ya Celtel na MultiChoice Tanzania watawagharamia vijana hao mafunzo kabla ya kwenda nchini Kenya kuwakilishi nchi katika mashindano hayo ya kuimba ambayo yanatarajiwa kufanyika Aprili 11, mwaka huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents