Michezo

Wayne Rooney aitikisa Man City Etihad (Video)

Mchezaji, Wayne Rooney wa klabu ya Everton inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya Sportpesa ameifungia bao timu yake dhidi ya Man City waliyokuwa nyumbani Etihad na kumfanya kutimiza idadi ya magoli 200 katika michezo ya ligi kuu.

Rooney anayekipiga The Toffes kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Manchester United ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipatia bao kabla ya City kurudisha bao hilo katika dakika ya 82 ya mchezo kupitia kwa Raheem Sterling na kuufanya kumalizika kwa matokeo ya 1-1.

Katika mchezo huo uliyokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika kwa timu zote mbili kusalia na wachezaji kumi baada ya wachezaji wao kupewa kadi nyekundu, kwa upande wa Everton alikuwa Morgan Schneiderlin wakati City ni beki wao City Kyle Walker.

Rooney ambaye ndie mfungaji wa muda wote ndani ya klabu ya United baada ya kuichezea michezo 559 na kufunga mabao 253 alirudi Everton tangu alipoondoka  miaka 13 iliyopita.

https://www.youtube.com/watch?v=vevRrN_2GU8&t=47s

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents