Michezo

Wayne Rooney akatwa mshahara

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imemlima adhabu ya kukatwa mishahara ya wiki mbili mshambuliaji wake, Wayne Rooney kufuatia kukutwa na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

Wayne Rooney

Makato ya fedha hizo zitapelekwa kwenye kituo cha watu wenye uhitaji maalumu nchini humo kama sera ya klabu ya Everton ya kusaidia watu wasiojiweza.

SOMA ZAIDI – Wayne Rooney ashushiwa ‘rungu zito’ na mahakama

Wayne Rooney ambaye anapokea kiasi cha Euro 150,000 kwa wiki itamlazimu kukatwa Euro laki 3, sawa na shilingi milioni 805  za kitanzania.

Mahakama nchini Uingereza siku ya Jumatatu ilimuhukumu Wayne Rooney kutoendesha gari kwa miaka miwili na kufanya kazi za kijamii kwa masaa 100 baada ya kukamatwa Septemba 1 akiwa anaendesha gari akiwa amelewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents