Aisee DSTV!

Wayne Rooney amjia juu Mourinho aponda kiwango chake na cha baadhi ya wachezaji ” Ana matarajio madogo”

Rooney amtupia dongo Mourinho

Mchezaji wa klabu ya DC United kutoka nchini Marekani Waynee Rooney amefuguka mwanzo mwisho kwa mara ya kwanza tangu aende Marekani kuhusiana na kocha wa United Jose Mourinho.

Mchezaji huyo wa DC aliongea hayo baada ya kuulizwa na mwandishi juu ya mwenendo wa klabu yake hiyo ya zamani ambao wanasua sua sana kwenye ligi kuu nchini Uingereza kwa kufanikiwa kucheza michezo 8 wakishinda minne wakipoteza miwili na kusuluhu miwili,tayari waki nafasi ya 8 kwa alama 13 mkononi huku wakiwa na tofauti ta alama 7 na timu inayoshikilia nafasi ya kwanza.

Rooney alisema ” Sio kitu kizuri kwa United wana wakati ngumu sana kwa wachezaji meneja wote kwa pamoja wana msimu mgumu sana,Namjua Mourinho ila kwa sasa amebeba mzigo mkubwa sana nilisema wiki chache zilizopita wachezaji wanatakiwa kusimama imara” aliongeza ” Wachezaji wanatakiwa wawe na mahesabu wanatakiwa kuwa bora zaidi kocha wanafanya mengi sana lakini yote yanakuwa ni wajibu wa wachezaji kuyafanyia kazi na kuleta matokea mazuri”

” Wana mwenendo mbaya sana,ni jukumu la kila mtu kuleta matokeo kwa pamoja lakini kwa upande wa Mourinho yeye pia ana matarajio madogo hana matarajio makubwa na timu hiyo” mbali na hilo kuna baadhi ya wachezaji wanatakiwa kuboresha viwango vyao wawe vizuri zaidi”

“Nilisema jambo lile lile wakati wa kocha Louis van Gaal alipokuwepo United,” alisema Rooney. “Nilisema, ‘Tunapaswa kufanya vizuri zaidi “.

Kwa upande wangu mimi naamini Van Gaal alituweka katika mfumo mzuri zaidi na alitutengenezea mazingira mazuri zaidi lakini sisi hatukuzalisha kile kilichotarajiwa ndo mana nikawa naongea nyuma ya kapeti kwamba tunapaswa kufanya vizuri ”

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW