Wazazi ‘wamtoa’ mtoto wao kafara

JESHI la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua mtoto wao kutokana na imani za kishirikiana.

Na Stella Ibengwe, Shinyanga




JESHI la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua mtoto wao kutokana na imani za kishirikiana.

Watuhumiwa hao ambao ni mtu na mkewe, ni Bw. Masakiliza Lukanya (31) na Bibi Nashoma Anthony (22), wakazi wa kijiji cha Songambele wanaodaiwa kumuua mtoto wao Milembe Masakiliza mwenye umri wa miezi mitatu.

Taarifa za awali zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 8 mwaka huu saa sita usiku, baba wa mtoto huyo aliporudi nyumbani na watu wengine watatu na kumwamuru mkewe awape watu hao mtoto.

Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alimwambia mkewe kuwa alikuwa akidaiwa mtoto tangu walipokuwa wakiishi kijiji cha Manigana kwa ajili ya kufanyiwa mazingara.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zilisema mwili wa mtoto huyo ulikutwa katika eneo la shamba umbali wa meta 50 kutoka nyumba ya wawili hao ukiwa umefukiwa katika shimo lenye kina cha futi moja huku umekatwa ulimi kwa mbele.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Shaibu Ibrahimu, daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu alithibitisha kuwa mtoto huyo aliuawa kwa kunyongwa shingo kwa mikono.

Taarifa zaidi za uchunguzi zilibaini kuwa baba mzazi wa marehemu kwa muda mrefu amekuwa haishi kwa waganga wa kienyeji akitafuta utajiri, hali iliyosababisha kumtoa kafara mwanawe huyo.

Kamanda Ibrahimu alisema Polisi inaendela kufanya uchunguzi ili kuwabaini waganga, wapiga ramli na watu waliokichukua na kukiua kichanga hicho, ili wote wachukuliwe hatua za kisheria.


 


Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents