Wazee wa masauti kukamua Bills

Wazee wa masauti kukamua Bills
Bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact ‘Wazee wa Masauti’, kesho
inatarajiwa kutoa burudani ya aina yake katika usiku wenye mahadhi ya
Kiafrika ‘Serengeti out of Africa’ kwenye ukumbi wa kimataifa wa Club
Bilicanas, jijini Dar es Salaam

Kwa mujibu wa Meneja Matukio wa
Club Bilicanas, Mohamed Bawazir, usiku huo utakuwa wa aina yake
kutokana na maandalizi ya bendi hiyo pamoja na burudani kutoka kwa madj
maarufu katika anga za uchezeshaji muziki.

Alisema Akudo Impact itatoa burudani ya nguvu huku madj maarufu
wakiwemo Dj Bike na DJ Ibra, ambao wataungurumisha disco la nguvu lenye
vionjo vya Kiafrika.

Bawazir alisema, programu ya madj itafuata baada ya Wazee wa Masauti kufanya vitu vyao.

Kuhusu kiingilio, alisema kitakuwa ni sh 5,000 na kiasi kingine kama
hicho mteja atalipa kwa ajili ya kuponi itakayomwezesha kupata vinywaji
au chakula ndani ya klabu kwa siku hiyo.

Aidha, wateja 100 wa kwanza, watapatiwa kinywaji cha Premium Serengeti
Lager bure, na kutoa wito kwa wateja kuwahi ofa hiyo, itakayotolewa na
wadhamini wa usiku huo, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

Meneja huyo alisema, wengine watakaopata zawadi za SBL ni wale
watakaovaa mavazi yanayorandana na ngozi ya chui, pia mwenye macho
yanayoshabihiana na macho ya chui, ambayo ni alama ya Serengeti Lager.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents