MichezoUncategorized

Wazee wa Simba wamuweka kitimoto Mo (Video)

Baada ya Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa kuingia makubaliano ya udhamini na klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kwa mkataba wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 4 za Kitanzania, mengi yameibuka ndani ya klabu hiyo.

Mohamed Dewji ‘Mo’ akiwa na mmoja kati ya viongozi wa Simba

Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye alikuwa mmoja kati ya wadhamini wakubwa wa klabu hiyo, aliwalaumu viongozi wa klabu hiyo kwa kuingia mkataba wa udhamini na kampuni hiyo bila ya yeye kupewa taarifa.

Baada ya kauli hiyo, Baraza la Wazee la Simba, limeibuka na kuzungumzia kauli hiyo huku wakidai mabadiliko ya katiba ya klabu hiyo yanafanyika kihuni.

https://youtu.be/Nt0Vz4SLhxc

Simba ilikuwa katika mchakato wa kubadili baadhi ya vipengele vya katiba ili iweze kuuza hisa zake kwa tajiri mfanyabiashara na mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ alishajitokeza kununua hisa asilimia 51 akiwekeza shilingi bilioni 20.

Akiongea na waandishi wa habari Alhamisi hii jijini Dar es salaam, Mratibu wa Baraza la Wazee la Simba, Felix Mapua, alisema kwamba wameamua kumuandikia barua Rais Magufuli, wakiomba kumuona.

“Tunaona mambo yanapelekwa haraka na kihuni, tumeamua kumuandikia barua Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa michezo, Dk Mwakyembe.

“Tunaomba kumuona Rais Magufuli, tunaona hata iwe kwa dharura. Hata kidogo hatukubaliani na mambo yanavyokwenda na hatufurahi hata kidogo.

“Simba ni kubwa sana, kubwa kuliko hata Mohamed Dewji. Hivyo hatuwezi kukubali mambo yaende namna hii,” alisema na kuongeza:

“Kuna wahuni wachache wanataka kupeleka mambo kibabaishaji, tunampa rais wetu Aveva kuwa aendelee na mwendo huu huu alionao, hapa kuna tatizo na ndiyo maana tayari tumesharipoti Takukuru juu ya hiki kinachoendelea.”

Baada ya hapo mwanachama mwingine wa klabu hiyo, aliyejitambulisha kwa jina la Bosi Matola mwenye kadi namba 080 alisema: “Kilichonileta hapa ni kumpongeza rais wangu Aveva kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo ya mapesa, kijana wetu Mo amelipa mishahara kwa miezi nane tu anaidai klabu shilingi bilioni 1.4, sasa angekaa miaka mitano si angechukua jengo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents