Tia Kitu. Pata Vituuz!

Waziri aeleza jinsi mgonjwa wa Corona alivyoingia Tanzania akitokea Ubelgiji, “Tunawatafuta aliokutana nao” – Video

Waziri aeleza jinsi mgonjwa wa Corona alivyoingia Tanzania akitokea Ubelgiji, "Tunawatafuta aliokutana nao" - Video

“Tarehe 15, Machi 2020 tulipokea msafiri Mtanzania mwanamke mwenye umri (46) ambaye aliwasili na ndege ya Rwandair akitokea Ubelgiji”.


“Msafiri aliondoka tarehe 3 Machi 2020th ambapo kati ya tarehe 5 hadi 13, Machi alitembelea nchi za Sweden na Denmark na kurudi tena Ubelgiji na kurejea nchini Machi 15, saa 10 jioni”.

“Msafiri alipita Uwanja wa KIA akafanyiwa ukaguzi na kuonekana kutokuwa na homa, baadae alianza kujisikia vibaya akiwa Hotelini na kwenda Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mt.Meru ambapo sampuli ilichukuliwa na kupelekwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii Dar es Salaam na vipimo vikathibitisha ana ugonjwa wa Corona (COVID-19)”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW