Aisee DSTV!
SwahiliFix

Waziri Jafo awapongeza wakazi wa Dar es Salaam

Mkoa wa Dar es salaam umekuwa kinara katika zoezi la uandikishaji wa orodha ya daftari la wapiga kura ambalo uandikishaji wake umefikia kilele Alhamis Oktoba 17.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mh. Selemani Jafo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mh. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma amesema awali mkoa huo ulianza kwa kusuasua, lakini baada ya hamasa wameweza kufanya vizuri na kufikisha asilimia 108.

“Niwapongeze wakazi wa Dar es Salaam wakati natangaza kwa mara ya kwanza mkoa huo ulikuwa na hali mbaya, lakini viongozi wa ngazi zote wamehamasishana na kufikia kiwango kikubwa,” amesema Mh. Jafo.

Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu wananchi wenye sifa ya kupiga kura ni 26,960,485, lakini lengo la kuandikisha wapiga kura lilikuwa milioni 22.9 sawa na asilimia 85, ya wananchi wenye sifa ya kupiga kura wanaume wakiwa 10,924,479 na wanawake 11,991,933.

Aidha amesema hadi kufikia Octoba 17 mwaka huu jumla ya wapigakura 19,681,259 walikuwa wamejiandikisha katika orodha ya daftari la wapigakura mwaka huu, kati yao wanaume ni 9,529,992 na wanawake 10,151,267, sawa na asilimia 86 ya lengo la wapigakura 22,916,412 ukiwa na mafanikio zaidi ukilinganisha na mwaka 2014.

Licha ya kila mkoa kuvuka lengo kwa asilimia 50,  mikoa mitano iliyoongoza ni Dar es Salaam 108%, Pwani 96%, Mwanza 95%, Tanga 90% na Singida 90% na kuzawadiwa kombe maalam.

Mikoa mitano ya mwisho licha ya kuvuka lengo ni Kigoma 65%, Njombe 75%, Simiyu na Shinyanga 76%, ambayo jumla ya Mkoa yote ni 86%.

CHANZO EATV

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW