Habari

Waziri Kabudi: China tuna wanafunzi zaidi ya 4000, wote wapo salama dhidi ya virusi vya CORONA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kuwa hakuna Mtanzania yeyote anayeishi nchini China, aliyekumbwa na maambukizi ya virusi vya homa ya Corona, vilivyozuka katika Mataifa ya Marekani, China, Thailand, Korea Kusini na Japan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.

Waziri Kabudi ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya hali ya Watanzania waishio nchini China na kusema kuwa Tanzania ina wanafunzi takribani 4000, ambapo katika mji wa Wuhan kuna wanafunzi 400 na kwamba kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania Nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki, ameihakikishia Serikali kuwa mpaka sasa hakuna mtanzania yeyote aliyeathiriwa ama kukumbwa na maradhi hayo.

Ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kujua maendeleo na hali za Watanzania wanaoishi jimboni Wuhan na China kwa ujumla na kuwataka Watanzania kuwa makini na suala la kutoa taarifa zisizo rasmi ama uvumi, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za Tanzania na kuwataka kuwa na subira ili kupata taarifa rasmi kutoka serikalini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents